• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Kairuki amshukuru Rais Samia

Imewekwa tarehe: November 24th, 2022

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan kwa kuchagiza maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye sekta ya elimu.

Waziri Kairuki ameyasema hayo leo Novemba 22, mwaka huu alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Manyara kwenye mkutano wa hadhara katika ziara ya kikazi ya Rais Samia.

Amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali kupitia fedha za UVIKO- 19 ilielekeza Sh.bilioni 300 kwa ajili ya kujenga madarasa 12,000 katika shule za Sekondari na madarasa 3000 kwa shule shikizi.

Waziri Kairuki ameeleza kuwa kupitia fedha hizo watoto 907,000 wameingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2022 na hakukuwa na mtoto aliyebaki nyumbani kusubiri awamu ya pili ya kuchaguliwa.

Amesema kuwa kupitia fedha hizo za UVIKO-19 Mkoa wa Manyara ulipata zaidi ya sh. bilioni 5.5 kwa ajili ya madarasa ya shule za sekondari, pia wamepata sh. bilioni 2 3 kwa ajili ya kujenga madarasa ya shule shikizi.

Aidha, Waziri Kairuki amesema Serikali imetoa kiasi cha sh. bilioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 8000 nchi nzima na kwa upande wa Mkoa wa Manyara umepata sh.bilioni 1.54 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 77 ili watoto wanaoingia kidato cha kwanza 2023.

Vile vile, Waziri Kairuki ameeleza kuwa kipitia mradi wa kuimarisha elimu ya sekondari nchini (Sequip) Sh.trilioni 1.2 zimetolewa ambapo mpaka sasa sh. bilioni 143.47 zimetumika katika ujenzi wa shule 2.32 katika mwaka wa fedha 2021/22.

Amesema katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali itajenga shule 184 katika Halmashauri zote ambapo kila shule itagharimu sh.milioni 600 lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa hakuna kata ambayo itakuwa haina shule ya Sekondari.

Aidha, amesema kuwa kwa miaka mitano Serikali itajenga shule 1026 kupitia mradi wa Sequip na kupitia mradi wa kuboresha elimu ya awali na msingi itaboresha madarasa zaidi ya 9000 yenye thamani ya sh. bilioni 250.9.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.