• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Lukuvi atoa suluhu mgogoro wa Mbuyuni, 1672 kumilikishwa

Imewekwa tarehe: August 16th, 2021

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameagiza wananchi 1,672 waliovamia maeneo na kuyaendeleza katika mtaa wa Mbuyuni kata ya Kizota mkoani Dodoma kupimiwa na kumilikishwa kulingana na jinsi walivyoendeleza na  ameonya tabia ya baadhi ya wananchi wanaovamia maeneo.

Aidha, ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Dodoma kuwachukulia hatua za kisheria watu 51 waliobainika kuhusika katika uuzaji maeneo kwa wananchi huku wakijua hawana umiliki wala mamlaka ya kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Mbuyuni leo tarehe 16 Agosti, 2021. Lukuvi alisema, uamuzi huo wa kuwabakisha wananchi waliovamia unafuatia ripoti aliyopewa na timu aliyoiunda kuchunguza mgogoro huo uliodumu kwa takriban miaka minne.

"Ninaagiza wananchi 1,672 waliovamia na kufanya maendelezo wapimiwe na kumilikishwa kulingana na ukubwa wa eneo la kila mmoja na yale maeneo ya wazi yaliyopimwa basi wapewe viwanja wananchi wengine 671’’ alisema Lukuvi.

“Maeneo mengi yanamilikiwa kwa hati na mtu anayejenga eneo la mtu ni mvamizi na wengi hapa Mtaa wa Mbuyuni mna sifa ya uvamizi na hata kama mtu hajaendeleza muda mrefu siyo sifa ya uvamizi’’ alisema Waziri wa Ardhi.

Timu iliyoundwa kuchunguza mgogoro huo ilipewa maelekezo ya kupokea na kusikiliza changamoto zote katika mtaa wa Mbuyuni, kubainisha aina ya vyanzo vya migogoro pamoja na kutambua uhalali wa nyaraka za umiliki.

Pia Tume hiyo ilikuwa na kazi ya kuhakiki hali ya maenedelezo yaliyofanyika, kubainisha majina na jinai iliyofanyika na mwisho kutoa mapendekezo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, wananchi wote watakaomilikishwa maeneo waliyoyaendeleza watatakiwa kulipa gharama za urasimishaji na wengine kulipa gharama kidogo za kufidia maeneo waliyovamia kwa lengo la kufidia waliochukuliwa maeneo yao kupata maeneo mengine.

Kuhusu maeneo ya viwanda, Waziri Lukuvi alitaka maeneo hayo kubaki kama yalivyopangwa na kuagiza wamiliki wake kuomba ujenzi wa viwanda kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Dodoma ndani ya siku tisini na wasipofanya hivyo watanyang’anywa maeneo hayo kwa mujibu wa sheria.

Aidha, Waziri Lukuvi aliwaaasa wananchi wa Dodoma kuhakikisha hawafanyi ujenzi wowote bila kupata kibali sambamba na kununua maeneo bila kuuliza mamlaka husika kwa kuwa kutofanya hivyo kunaweza kusababisha kuuziwa maeneo yaliyopangwa kwa matumizi ya huduma za jamii.

"Msijenge wala kununua eneo bila kuulizia mamlaka husika na ujenzi lazima uwe na kibali maana mamlaka ya upangaji ni ya jiji la Dodoma" alisema Lukuvi.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka alimuahidi Waziri Lukuvi kusimamia utekelezaji wa maagizo yote yaliyopendekezwa kwenye ripoti na kumtaka Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri kuhakikisha anasimamia na kutatua changamoto zote za ardhi badala ya kuacha changamoto kupelekwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Mmoja wa wananchi wa Mtaa Mbuyuni katika kata ya Kizota aliyejitambulisha kwa jina la Mtumishi Yohana ameunga mkono uamuzi wa Waziri Lukuvi kwa kueleza kuwa ana imani sasa haki itatendeka katika eneo hilo.

Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Mbuyuni Kata ya Kizota waliojitokeza kumsikiliza Waziri Lukuzi akitoa maamuzi baada ya kupata taarifa kutoka tume iliyoiunda ili kupata suhuhisho la mgogoro wa eneo hilo. 

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.