• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Mhagama aagiza muongozo Lishe uanze Julai

Imewekwa tarehe: June 8th, 2021

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama ameziagiza Taasisi za TFNC, MUHAS, SUA na TBS kuharakisha uandaaji wa muongozo wa lishe ili uanze kutumika kuanzia mwezi Julai, 2021

Waziri Mhagama ametoa agizo hilo alipotembelea na kukagua utekelezaji wa  mradi wa Boresha Lishe katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Julai 6, 2021

“Jambo hili limeingia kwenye programu ya kwanza ya boresha lishe ninaomba Watanzania wote tushukuru, tuunge mkono na hatuna haja ya kuchelewa tena na muongozo huu utoke kabla ya mpango wa pili haujaanza” Aliongeza Waziri Mhagama.

Amesema kuwa muongozo huo utaliondoa Taifa kwenye tatizo la udumavu kwa kiasi kikubwa sana kama kila mtu atajenga tabia ya kunywa uji wa lishe bora.

“Tujenge tabia ya kunywa kikombe cha lishe kila asubuhi, wafanyakazi wanywe, wanafunzi wanywe, uji huu utabadilisha mtazamo na kuboresha afya za watoto, wakubwa na wazee wote kwani wanahitaji kuwa na lishe bora, mimi mwenyewe nitaongoza kampeni ya kunywa uji wa lishe asubuhi” Alisisitiza Waziri Mhagama.

Aidha, amesema mradi huo umeweza kuongeza wanawake wanaokula vyakula mchanganyiko ambavyo ni vya asili kutoka asilimia 17 mpaka asilimia 49.

Pia idadi ya watoto kutoka miezi 6 - 23 wanaopata vyakula mchanganyiko imeongezeka kutoka asilimia 3 mpaka 35 na kusisitiza kuwa mradi huu umekuwa na faida kubwa sana.

Katika ziara hiyo Waziri Mhagama alikabidhi pampu 75 za umwagiliaji kwa ajili ya visima vifupi vilivojengwa na mradi huo pamoja na mashine za kushonea 40 kwa ajili ya vikundi vya VICOBA na pia alitembelea kijiji cha Buigiri ambapo alijionea shughuli za ushonaji, bustani za mboga mboga, maonyesho ya mapishi na vibuyu chirizi.

Kwa upande wake Meneja miradi wa WFP Bi. Alessia Decaterina amesema wamefanikisha mradi wa boresha lishe katika  wilaya nne za Bahi, Chamwino, Ikungi na Singida Vijijini na mradi huo umekuwa na faida kubwa sana kwa wakazi wa maeneo hayo na kusisitiza kuwe na uendelevu katika kusimamia miradi iyo ili izidi kufaidisha watu wengi zaidi.

Mradi wa Boresha Lishe unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani na kufadhiliwa kwa pamoja na Umoja wa Ulaya ukilenga kuimarisha upatikanaji na matumizi ya chakula chenye lishe kwa wanawake na watoto kupitia mabadiliko ya tabia, kuzalisha vyakula mchanganyiko na kusambaza chakula bora katika Wilaya za Bahi na Chamwino mkoani Dodoma na Wilaya za Ikungi na Singida Vijijini Mkoani Singida.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma atoa pongezi kwa Madiwani

    May 25, 2025
  • Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

    May 23, 2025
  • Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

    May 23, 2025
  • Wananchi Kata ya Madukani washukuru kuboreshwa huduma za Afya, Zahanati ya Chikande

    May 21, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.