• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Mkenda awaita wawekezaji Hoteli Dodoma

Imewekwa tarehe: May 11th, 2021

SERIKALI amewaasa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika sekta ya Hoteli Jijini Dodoma kutokana na fursa zilizopo zinazoendana na kukua kwa Jiji hilo.

Ameyasema hayo Mei 8, 2021 na Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda, wakati akizundua hoteli ya Rafiki Dodoma Hotel yenye hadhi ya nyota nne iliyojengwa na muwekezaji mzawa Bw. Fladmiry Mallya kutoka Rombo mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mkenda amesema kuwa wawekezaji wanahitaji katika jiji la Dodoma kutokana na uwepo wa shughuli nyingi za kiserikali na kitaifa ambazo zinahitaji uwekezaji katika huduma mbalimbali.

Akizungumzia uzinduzi wa Hoteli hiyo Prof. Mkenda amesema kuwa itasaidia kupunguza changamoto ya nyumba za kulala wageni zenye hadhi ambazo zinahitajika hivi sasa kwa wingi jijini Dodoma.

“Kupatikana kwa hoteli hii katika jiji la Dodoma itatusaidia kuondoa usumbufu uliokuwepo hapo awali hasa wakati wa mikutano mikubwa ambayo wageni walikuwa wanapata shida kupata sehemu ya za kulala zenye hadhi” amesema Prof. Mkenda.

Aidha, Prof. Mkenda amesema kuwa wawekezaji wote ambao wanataka kuja kuweza katika jiji la Dodoma milango ipo wazi kwani serikali itasaidia kufanikisha uwekezaji wao ili kusaidia kutoa ajira kwa makundi mbalimbali.

Pia amesema kuwa kwa sasa serikali imeweka mazingira wezeshi kwa mtu yeyote ambaye atahitaji kuja kuweza katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake Mbunge wa Dodoma, Antony Mavunde amesema kuwa jiji la Dodoma limejipanga kuhudumia wawekezaji ambao wataonyesha nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali.

Mhe. Mavunde amesema kuwa hivi sasa kupitia baraza la madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, wameweka mikakati ya kuhudumia wawekezaji kwa muda mfupi na kuwapatia maeneo ya uwekezaji bila urasimu.

“Moja ya faida ya uwekezaji kama huu hapa jijini Dodoma ni kubadili muonekanao wa jiji letu lakini pia uwepo wa hoteli kubwa kama hivi kunasaidia kuondoa uhaba wa nyumba za kulala wageni hasa wakati ule tunapokuwa na mikutano mikubwa.

Naye Mkurugenzi wa Hoteli hiyo, Fladimiry Mallya, amesema kuwa anategemea kupata wageni wengi kutokana na huduma bora wanazotoa katika Hoteli hiyo ya kisasa katika Jiji la Dodoma.

Hata hivyo, ametoa wito kwa  serikali kuwashika mkono wawekezaji katika kuwasaidia kukabiliana na kero mbalimbali ambazo wamekuwa wakikumbana nazo.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.