• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Mkuu aagiza Jiji la Dodoma, LATRA kukutana

Imewekwa tarehe: November 24th, 2022

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa Jiji la Dodoma ukutane na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) ili kutengeneza mpangilio wa safari za daladala ndani ya jiji hilo kuelekea soko jipya la wajasiriamali wadogo lililoko barabara ya Bahi. 

Ametoa maagizo hayo leo (Alhamisi Novemba 24, 2022) mara baada ya kutembelea na kukagua soko jipya la wajasiriamali wadogo lililoko eneo la Bahi Road jijini Dodoma.

Mhe. Majaliwa amesema sambamba na utekelezaji wa maagizo hayo Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) mkoa wa Dodoma wanatakiwa kuhakikisha wanafanya maboresho ya stendi ili iweze kukidhi viwango vya kupokea magari ya abiria yatakayoelekezwa eneo hilo kwa kuboresha barabara inayopita nyumba ya soko ili kuimarisha njia za usafiri.

Pia, ameitaka Halmashauri ya Jiji la Dodoma isimamie utoaji wa fedha za mikopo kwa wafanyabiashara walioko katika soko hilo ili waongeze mitaji na kukuza biasharazao.   “Nataka nipongeze uamuzi wenu (wafanyabiashara wadogo) wa kuja hapa mmefanya maamuzi sahihi na mtanufaika.” amesema Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa.

Aidha, Mhe. Majaliwa amesema kuwa ni dhamira ya dhati ya Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kuwainua wafanyabiashara wadogo kwa kufungua milango ya ufanyaji biashara kwa uwazi na Serikali kuwapa huduma muhimu zitakazowasaidia kuleta tija kwenye shughuli zao.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuhakikisha anafanyia kazi changamoto zilizojitokeza baada ya wafanyabiashara wadogo wadogo kuhamia katika eneo hilo ikiwemo kuweka vikingia mvua na kwa kushirikiana na TARURA kuweka taa za barabarani.

Awali akijibu maombi ya wafanyabiashara hao, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru amesema Halmashauri ya Jiji imetenga Shilingi Milioni 400 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wafanyabiashara walioko sokoni hapo na hadi kufikia mwezi Disemba mwaka huu watakuwa wameshakamilisha taratibu za utoaji wa mikopo hiyo.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Festo Dugange amesema ujenzi wa soko hilo ni dhamira njema ya Rais Samia Sulluhu Hassan ya kuwajali na kuwapenda wafanyabiashara wadogo wadogo ili waondokane na adha ya kutembea na bidhaa zao badala yake wapate sehemu nzuri na bora ya kufanya biashara zao.


Matangazo

  • TANGAZO LA MABADILIKO YA TAREHE YA USAHILI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA WASIMAMIZI JIMBO LA MTUMBA October 03, 2025
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA- DODOMA MJINI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA MAKARANI WAOGOZAJI WAPIGA KURA October 03, 2025
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Rc Senyamule awasihi wawekezaji sekta binafsi kuwekeza Dodoma

    October 03, 2025
  • CCTV kamera mwarobaini wa wavunjifu wa sheria jiji la Dodoma

    October 02, 2025
  • Wadau wa afya wapongezwa kwa juhudi zakudhibiti vifo vya wajawazito

    October 01, 2025
  • UONGOZI WA KLABU YA MICHEZO OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAKUTANA NA RAS KAZUNGU

    September 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.