WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wawekezaji kuwaalika marafiki zao nje ya mipaka ya Tanzania kuja kuwekeza Tanzania kwa kuwa kuna miundombinu rafiki katika sekta ya uwekezaji nchini.
Aliyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua kiwanda cha kuunganisha magari cha GF-Vehicle Assembling kilichopo Kibaha mkoni Pwani na kuwahakikishia wawekezaji nchini kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono katika jitihada zao za uwekezaji kwa kuhakikisha hawapati changamoto.
Aidha amesema kuwa zile changamoto zitakazojitokeza na zinazopo ndani ya uwezo wa Serikali basi Serikali itazisimamia na kuzitatua ili waweze kuendelea kufanya vizuri .
Pia ameupongeza mkoa wa Pwani kwa kutumia fursa ya maendeleo ya viwanda nchini ambapo kwanza umeweza kutenga maeneo mengi ya ardhi katika halmashauri zake zote na kuvutia wawekezaji wengi.
Awali Mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo ameeleza kuwa mkoa huo ni wa viwanda ambapo hadi leo vimefikia 1,438 kati yake vikubwa kama hicho alichotembelea ni zaidi ya 82.
Kwa Upande wa mkurugenzi wa kiwanda hicho Ali Jawad Karmali alisema wao kama GFA Wanajivunia kuwekeza nchini Tanzania na kuwa kiwanda cha kwanza kutengeneza magari nchini.
Pia Karmali aliiomba serikali kupitia taasisi zake ikiwemo majeshi na iwape kazi ya kutengeneza magari yao badala ya kuagiza gari kamili waagize vipuli na jukumu la kuunganisha liwe juu yao.
Vile vile alisisitiza kuwa anaamini changamoto ndogo ndogo wanazo kutana nazo zitatatuliwa kwa kushirikiana na serikali. Kampuni hiyo imetoa ajira zaidi ya 100 kwa watanzania ambao zimegawanyika katika sehemu 3 za kugumu, mikataba na za muda mfupi alimalizia Karmali.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.