WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameipongeza benki ya NMB kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na taasisi za Serikali katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya.
Mhe. Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatatu, Septemba 6, 2021) wakati akizindua Asasi ya Kiraia ya NMB. Uzinduzi huo umefanyika katika Hotel ya Kilimanjaro Hyatt jijini Dar es Salaam.
“Nitoe wito kwa taasisi nyingine za fedha na zisizo za kifedha na hata mtu mmoja mmoja kujenga utaratibu wa kurejesha kile kidogo alichoturuzuku Mwenyezi Mungu kwa jamii.”
Waziri Mkuu amesema Serikali inaunga mkono jitihada hizo ambazo zinalenga kupunguza changamoto katika maeneo ya afya, elimu, kilimo, mazingira na ujasiriamali nchini.
Amesema Serikali inaamini kuwa, kuanzishwa kwa asasi hiyo kutaimarisha utoaji wa huduma za kijamii. “Hiki ni kielelezo tosha kuhusu kujitoa kwa NMB kwa jamii inayotuzunguka.”
Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna alisema asasi hiyo inalenga kusimamia na kufuatilia maendeleo ya jamii katika sekta za elimu, afya, kilimo, mazingira na ujasiriamali.
Aliongeza kuwa mbali na asasi hiyo pia benki hiyo imeanzisha mpango maalumu wa kutoa ufadhili wa masomo ya kidato cha tano na sita pamoja na vyuo vikuu kwa wanafunzi wenye ufaulu wa juu lakini wanatoka katika mazingira magumu. “Kwa mwaka huu tutaanza na wanafunzi 200.”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.