Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Julai 03, 2023 amekagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Akizungumza baada ya kukagua ujenzi huo, Mheshimiwa Majaliwa ameagiza kuwa ifikapo Oktoba mwaka huu, majengo hayo yawe yamekamilika na kuwekwa samani, ili azma ya Serikali ya watumishi kuhamia kwenye majengo hayo ifikapo Januari Mosi, 2024 itimie.
“Dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kutaka kuona watumishi wote waliohamia Dodoma wanafanya kazi kwenye majengo rasmi fedha imetengwa, imetolewa na itaendelea kutolewa”
“Tafuteni mbinu za kiufundi za kukamilisha majengo haya kwa wakati bila kuathiri viwango”Moja ya mbinu ni kusimamia ujenzi huu usiku na mchana, tunataka tumalize majengo haya, Watanzania wanataka kuona majengo yanakamilika na kutumika.”
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wasimamizi wa ujenzi wa majengo kwenye mji wa Serikali watumie bidhaa zinazozalishwa na viwanda vilivyopo nchini“. Rais Dkt. Samia amesisitiza kuhusu uwekezaji na amekuwa akialika wawekezaji wa nje na wa ndani kujenga viwanda vya bidhaa mbalimbali hapa nchini ikiwemo marumaru (tiles). Tutumie bidhaa zao badala ya kuagiza bidhaa hizo kutoka nje.”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.