WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo amekagua uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ambao utatumika kwa sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo kesho. Rais Mteule Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuapishwa kesho ili kuanza muhula wa pili wa Serikali ya awamu ya tano baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu iliofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza Dkt. Magufuli kuwa mshindi kwa asilimia 84.4 ya kura zote zilizopigwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwia akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakati alipowasiri kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma leo kukagua maandalizi ya uwanja huo utakaotumika kwa shughuli za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.