• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Mkuu asimamisha likizo, madarasa yakamilike

Imewekwa tarehe: December 7th, 2020

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini wahakikishe kuwa watendaji wote wa Mikoa, Wilaya, Halmashauri wasiende likizo ya sikukuu ya Krismas na mwaka mpya kwa mwaka huu, badala yake wakasimamie ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na madawati na wawe wamekamilisha ifikapo mwezi Februari 28, 2020.

“Suala hili nitalifuatilia mwenyewe ili kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa chagua la kwanza na la pili wawe wameingia madarasani kufikia Machi mosi mwaka 2021. Ukamilishaji wa vyumba hivyo Pamoja na madawati ufanyike kwa kutumia vyanzo vyenu vya ndani vya fedha”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo Jumatatu Disemba 7, 2020 alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI. Kikao hicho ambacho Waziri Mkuu alikiongoza kwa njia ya televisheni akiwa ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma kilihusu upokeaji wa taarifa ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 2021.

Waziri Mkuu ameiagiza Ofisi ya Rais-TAMISEMI ihakikishe kazi hiyo inakamilika kwa wakati na amewataka watendaji hao wahakikishe ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa na utengenezaji wa madawati nafanyika usiku na mchana.

Awali, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Gerald Mweri alisema kati ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021, wanafunzi 970 watapangwa kwenye shule maalum, 1,059 shule za ufundi, 1,280 bweni kawaida, 803,326 watapangwa katika shule za sekondari za kutwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera alisema katika mkoa wake wanafunzi wote waliofaulu watapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza 2021 kwa sababu awali walikuwa na upungufu wa vyumba 42 vya madarasa, ambapo wamejenga shule mpya saba zenye vyumba 26 vya madarasa na wamekamilisha maboma 56 na hivyo kuw na ziada ya vyumba 36 vya madarasa.

Kiongozi huyo alisema kuwa mkoa umeweka mkakati wa kuwapeleka wanafunzi wote waliofeli katika vyuo vya maendeleo ya wananchi ili kuwawezesha kujitegemea. “Mpango huu tunautekeleza kwa awam ya pili sasa”.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema kuwa mkoa wake ulikuwa na upungufu wa vyumba 400 vya madarasa, hadi sasa tayari wamekamilisha ujenzi wa vyumba 380 na kwamba watahakikisha hadi Januari 30, 2021 watakuwa wamekamilisha ujenzi wa vyumba vilivyosalia na wanafunzi wote watachaguliwa katika awamu ya kwanza.

Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara ikamilishe utaratibu wa kuwa na bei kikomo ya saruji ili kuuwezesha kila mkoa kujua bidhaa hiyo inapaswa kuuzwa kwa bei gani kwa ania ya kuondoa upandishwaji holela unaofanywa na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka Mawakala wabadilike na waachane na tabia ya kuficha bidhaa kwa ajili ya  kuzipandisha bei, kwani mtu yeyote akikutwa anatengeneza mazingira ya kufanya bidhaa isipatikane kwa lengo la kupandisha bei huo ni uhujumu uchumi na ikiwa atakutwa na bidhaa ambayo inatafutwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.