• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Mkuu azindua kiwanda cha kuchakata maziwa Nsimbo

Imewekwa tarehe: December 14th, 2022

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua kiwanda cha kuchakata maziwa cha MSS kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Mkoani Katavi ambacho kina uwezo wa kusindika wastani wa lita 10,000 kwa saa.

Akizungumza baada ya kuzindua kiwanda hicho ambacho uwekezaji wake umegharimu shilingi milioni 600, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kila mwenye uwezo awekeze.

Amesema hayo wakati akizungumza na wananchi baada ya kuzindua kiwanda hicho ambacho kwa sasa kinazalisha maziwa ya mtindi na maziwa fresh na kinatarajia kuanza uzalishaji wa Samli hivi karibuni.

Pia,Majaliwa ametoa rai kwa wafugaji wanaozunguka kiwanda hicho kuuza maziwa kwa mwekezaji huyo ili waweze kujiongezea kipato na kumwezesha mwekezaji huyo kuwa na uhakika wa malighafi ya kutosha.

“Huyu Bwana Maliki anamuunga mkono Rais Mheshimiwa Dkt. Samia katika nia yake ya kuendeleza uwekezaji nchini. Uwepo wa kiwanda hiki kunaisaidia kuendeleza  mkakati wa lishe bora kwa kila Mtanzania, kwa sasa tunamshauri aendelee kupanua kiwanda hiki ili aongeze uzalishaji na wananchi wengi wazidi kupata ajira.”

Awali, Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi inayojengwa katika eneo la Ilembo, Mpanda, ambapo alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya sita imeendelea na mkakati wa kupeleka huduma karibu na wananchi kwa kuhakikisha inajenga majengo ya ofisi ya mikoa na wilaya mpya  Katavi ukiwemo.

Aidha,alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wananchi kwamba Serikali yao itaendelea kuwatumikia, hivyo waendelee kuiamini na kuiunga mkono. “Serikali itaendelea kuwatumikia na haitowaangusha sisi wasaidizi wa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia tutafanya kazi wakati wote, wakati wa jua kali na hata wakati wa mvua, tunataka kuhakikisha dhamira ya Rais wetu ya kuleta maendeleo inatimia.”

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alisema kuwa Rais Dkt. Samia ameridhia kutoa shilingi milioni 200 kupitia Bodi ya Maziwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha ukusanyaji wa maziwa Mpanda, Katavi. “Vituo hivi vitajengwa takribani kumi nchi nzima na kila kimoja kitagharimu shilingi milioni 200.”

Ameongeza kuwa Rais Dkt. Samia ametoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa mitamba ya maziwa 500 na madume ya nyama 500 ambayo yatagawiwa nchi nzima, lengo likiwa ni kuboresha aina ya mifugo inayofugwa na wananchi. “Serikali inataka wananchi wafuge kisasa na kibiashara.”

Naye, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Geofrey Pinda alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini {DPP} kufanya mapitio ya kesi na  majalada mbalimbali ili yasiyokuwa na mashiko au ushahidi wa kutosha yaondolewa ili wahusika  wakaendelee na shughuli za uzalishaji mali.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.