• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Mkuu Majaliwa aagiza kila Afisa Ugani kuwa na shamba darasa

Imewekwa tarehe: June 14th, 2021

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI wahakikishe Maafisa Ugani wote nchini wanakuwa na mashamba darasa kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wakulima katika maeneo yao.

“Maafisa Ugani lazima wawe na mashamba kwa ajili ya kufundishia wakulima na Afisa Ugani anayeshindwa kuonesha shamba huyo hafai kuwa Afisa Ugani.”

Ametoa agizo hilo jana (Jumapili, Juni 13, 2021) wakati akizungumza na wadau wa zao la alizeti katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Mafunzo ya Kanisa Katoliki, Mkoani Singida.

Waziri Mkuu alisema wananchi waliacha kulima kwa sababu elimu ilikuwa haiwafikii, hivyo amewaagiza Wakuu wa Wilaya katika maeneo yote yanayolima alizeti wasimamie uundwaji wa vikundi vya wakulima wa zao hilo. “Vikundi ndio njia rahisi ya kuwafikia wakulima iwe kwa kuwapa elimu au mikopo.”

“…Hakikisheni mnakuwa na kanzidata za wakulima katika maeneo yenu. Kanzidata hiyo itawawezesha kujua idadi ya wakulima, ukubwa wa mashamba yao pamoja na mahitaji yao. Pia jengeni utaratibu wa kuwatembelea wakulima ili kujua changamoto zinazowakabili na kushirikiana nao katika kuzitafutia ufumbuzi.”

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwaagiza viongozi wa mikoa yote nchini waandae mpango mkakati wa kuendeleza mazao ya mafuta na kuuwasilisha Wizara ya Kilimo kwa ajili ya uratibu, usimamizi na ufuatiliaji. “Na kila kiongozi anapofanya ziara katika wilaya asomewe taarifa kuhusu hatua waliyofikia.”

“Halmashauri za Wilaya zitenge maeneo ya kuzalisha mbegu bora na kuanzisha mashamba makubwa ya pamoja (Block farms) ili kuongeza uzalishaji na kurahisisha utoaji wa huduma za ugani, mitaji na upatikanaji wa malighafi kwa viwanda vya mafuta ya kula.”

Kadhalika, Waziri Mkuu alizielekeza taasisi za utafiti wa masuala ya kilimo ziendelee kufanya tafiti za udongo ili kubaini ni aina gani ya mbegu zinazofaa kupandwa kwenye eneo husika. Amesema tafiti zinawawezesha wakulima kupanda mbegu sahihi katika mashamba yao, hivyo kupata mavuno mengi na bora.

Naye, Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema wizara imejipanga katika kuongeza uzalishaji wa mbegu bora kutoka tani 344 za sasa hadi kufikia wastani wa tani 2,000 hadi 2,500 kwa mwaka, hivyo ndani ya miaka mitatu ijayo nchi itakuwa imejitosheleza kwa mahitaji ya mbegu bora za alizeti.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Binilith Mahenge aliiomba Serikali kuunda bodi itakayosimamia mazao ya mafuta ili kuboresha usimamizi wa mazao hayo. Pia aliishauri Serikali kupitia taasisi zake kama Jeshi la Magereza zianzishe mashamba ya mbegu za alizeti ili kurahisisha upatikanaji wake.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.