WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewasili nchini Morocco kwa ziara ya kikazi Julai 12, 2021.
Akiwasili katika uwanja wa Mohammed V jijini Casablanca Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokelewa na Waziri Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa Morroco Mohcine Jazouli
Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha mahusiano hususani ya kiuchumi kati ya Tanzania na Morocco.
Katika ziara hiyo Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor, Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda na Mkurgenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Japhet Justine.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.