WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene ameongoza kikao cha Mawaziri kujadili mbinu ya kutatua na kukabili vitendo vya ukatili kwa watoto na Wanawake linaloendelea katika Jamii.
Katika kikao hicho kilichofanyikaJijini Dodoma kimehusisha Mawaziri mbalimbali wakiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolph Mkenda, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angela Kairuki, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Geofrey Pinda.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amewaomba Mawaziri ushirikiano kuhakikisha changamoto hiyo inapungua au kuisha kabisa kwa kuweka mpango wa muda mfupi na mrefu kwa pamoja.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.