Na. Dennis Gondwe, DODOMA
WILAYA ya Dodoma ilipokea shilingi 9,539,477,529 kwa ajili ya maendeleo zilizotumika kujenga miundombinu ya elimu msingi na sekondari na kuchangia katika ukuaji sekta hiyo na kuongeza ufaulu.
Taarifa hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi alipokuwa akisoma risala ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma katika uwanja wa Shule ya Msingi Chamwino jijini hapa.
Mbugi alisema “Mheshimiwa Rais; katika kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023, Wilaya ilipokea shilingi 9,539,477,529.06 kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya elimu. Kati ya fedha hizo, shilingi 3,456,608,415.29 za elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari na shilingi 6,082,869,113.77 zilitumika kujenga miundombinu katika shule za msingi na sekondari”.
Akiongelea uboreshaji mazingira ya kujifunzia na kufundishia alisema kuwa yameboreka. “Mheshimiwa Rais; kuboreshwa kwa mazingira ya kujifunzia na kufundishia kumeongeza ufaulu shule za msingi kutoka asilimia 89.2 mwaka 2021 hadi asilimia 89.9 mwaka 2022. Pia wanafunzi 13,667 waliandikishwa kwa mwaka 2023 kujiunga na darasa la awali, sawa na asilimia 89.7, wanafunzi 19,508 waliandikishwa kwa mwaka 2023 kujiunga na Darasa la kwanza sawa na asilimia 103.3. Katika shule za sekondari udahili wa wanafunzi wa kidato cha kwanza uliongezeka kutoka asilimia 86 mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 88.7 mwaka 2023, Kidato cha Nne ufaulu uliongezeka kutoka asilimia 92.8 mwaka 2021 hadi asilimia 95.2 mwaka 2022 na kidato cha Sita umeongezeka kutoka asilimia 99.9 mwaka 2022 hadi asilimia 100 mwaka 2023” alisema Mbugi.
Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 unaongozwa na kaulimbiu isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa ustawi wa Viumbe Hai kwa Uchumi wa Taifa”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.