• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wizara yaanza Kampeni Mkoa kwa Mkoa kupinga vitendo vya ukatili nchini

Imewekwa tarehe: October 19th, 2022

WIZARA ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta na wadau wa Maendeleo imeanza Kampeni maalum ya Mkoa kwa mkoa kupambana na vitendo vya ukatili.

Akizungumza wakati wa kilele cha kampeni ya kupinga ukeketaji mkoani Manyara, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Wakili Msomi Amon Mpanju amesema Wizara imeamua kuweka nguvu hasa katika kutoa elimu katika ngazi za Mkoa, Halmashauri, Kata, mitaa na vijijini ili kusaidia jamii kuondokana na vitendo vya ukatili.

Wakili Mpanju ameongeza kuwa kuharibika kwa misingi ya malezi bora katika jamii juu ya suala la malezi na makuzi imeelezwa kuwa chanzo cha ukatili ndani ya Jamii hivyo jamii inaoaswa kuzingatia swala la malezi na kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili.

Pia Wakili Mpanju ameitaka jamii ya mkoa wa Manyara kuunga mkono jitihada za Serikali na wadau za kupambana na ukatili wa ukeketaji nchini kwani wao ni ndio njia pekee ya kuondokana na vitendo hivyo.

Ameongeza kuwa Serikali pia inaweka mkakati katika kuhakikisha jamii inapata uelewa wa namna  bora kuwalinda watoto wao dhidi ya vitendo vya ukatili kwa kuanzisha Mwongozo wa Kuunda Madawati ya Ulinzi wa Mtoto shuleni unaosaidia kuwa na sehemu maalum kwa watoto kuripoti viashiria au wanapofanyiwa vitendo vya ukatili.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema Mkoa umejipanga thabiti katika kuifikia jamii na kutoa elimu kupitia Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii ili kujenga uelewa wa madhara na matatizo ya watoto wa kike kufanyiwa vitendo vya ukeketaji ambavyo ni miongoni mwa vitendo vya ukatili.

"Sisi tunawashukuru Wizara kwa kutuunga mkono katika mapambano haya dhidi ya ukeketaji mkoani hapa sio jambo rahisi sisi tutaendelea kuweka msisitizo katika elimu kwa jamii hasa watoto wa kike na wa kiume ili wawe mabalozi wazuri wa kupambana na ukeketaji katika jamii" alisema Mhe. Twange.

Naye Mwakilishi wa Dawati la Jinsia Polisi Makao Makuu Mariam Kipesa amesema Jeshi la Polisi kupitia Dawati hilo limeweka mikakati ya makusudi ili kuhakikisha ukatili hasa ukeketaji unatokomezwa kwa kuunganisha nguvu ya pamoja baina ya Jeshi hilo wananchi na wadau wengine ili kukiokoa kizazi cha watoto wa kike nchini.

Kwa upande wake Mbunge wa Simanjiro mkoani Manyara Christopher Olesendeka ameitaka jamii ya Manyara kuendeleza Kampeni ya kupinga ukeketaji katika mitaa na vijijini vyao ili kuweza kukabiliana na vitendo hivyo hasa kupata uelewa wafanye nini wanapoona viashiria au kutokea kwa vitendo hivyo vya ukatili hasa ukeketaji.

Aidha Mwakilishi wa UNFPA Dkt. Majaliwa Marwa amesema Kampeni itakuwa chachu ya kupunguza au kutokomeza vitendo vya ukeketaji na ameishukuru Serikali kwa kuweka Mkakati wa kutokomeza ukeketaji kwani inaonyesha dhamira ya Serikali katika kutokomeza ukeketaji na jitihada za kutokomeza ukeketaji zinaanza na msichana mmoja mmoja, jamii na nchi nzima.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.