• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wizara yaja na mwarobaini wa migogoro ya ardhi Dodoma

Imewekwa tarehe: June 30th, 2023

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeongeza Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dodoma atakayeshughulikia Halmashauri ya Jiji la Dodoma ili kukabiliana na changamoto za ardhi jijini hapo.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula alipokuwa akiongea na wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wenye changamoto za kupewa ‘control number’ na madai ya hatimiliki yaliyochukua muda mrefu katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Dkt. Mabula alisema “kutokana na changamoto ya migogoro ya ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, tunakwenda kuongeza Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dodoma atakayeshughulikia Halmashauri ya Jiji la Dodoma pekee ili kumpunguzia mzigo wa Halmashauri nyingine za Mkoa wa Dodoma”.

Akiongelea maelekezo yake kwa wataalam wa ardhi, alisema kuwa aliwaelekeza kupanga ratiba ya siku mbili kwa wiki, siku ya Jumanne na Ijumaa kutoka ofisini kwenda katika maeneo ya watu badala ya wananchi kuwafuata ofisini. “Leo nimekuja kusikiliza wananchi ambao wamekalimisha taratibu na malipo ya halmashauri lakini wanahitaji ‘Control number’ kwa ajili ya malipo ya wizara…, Pili wananchi ambao walishakamilisha taratibu zote lakini hatimiliki zao hawajapatiwa” alisema Dkt. Mabula.

Akiongelea migogoro iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Waziri aliitaja kuwa ni migogoro inayotokana na fidia. “Wananchi maeneo yao yalichukuliwa kwa ajili ya maendeleo ya Dodoma tunayoyaona hapa na hawajalipwa fidia zao. Changamoto nyingine ni upimaji shirikishi wa mgawanyo wa asilimia 70 kwa 30. Upimaji huu haukwenda katika utaratibu ule tuliokuwa tunautegemea kama mkoa na halmashauri nyingine zilivyofanya. Nyingine ni ‘double allocation’. Viwanja vilivyokuwa vimemilikishwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) na wataalam wetu wa Halmashauri wakavimilikisha tena watu wengine. Matokeo yake kukawa na migogoro” alisema Dkt. Mabula.

Migogoro mingine inatokana na watanzania kutokuwa na uelewa wa sheria ya Ardhi na migogoro wanayokuwa nayo na hatua ya kutatua migogoro hiyo. “Sisi kama wizara kazi yetu ni kusimamia utekelezaji wa sera na sheria. Utekelezaji wa mpango wa matumizi ya Ardhi na mamlaka ya upangaji miji ni Halmashauri ya Jiji la Dodoma na halmashauri nyingine. Wananchi wamekuwa wakija wizarani kuwasilisha malalamiko yao. Lakini kwa sababu tupo wote Dodoma, tunafanya kazi kama timu moja kwa sababu serikali ni moja” alisema.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alisema kuwa jiji lake linatakiwa kufidia wananchi takribani viwanja 3,995. “Viwanja 1,035 vipo eneo la Nala, tumeamua kwenda kurejesha viwanja 1,035 kwa wananchi kwa maana ya kwenda kupunguza kwenye viwanja 3,995 na Kamati ya Ugawaji Ardhi imeshakaa kwa hiyo tutakualika kuja kukabidhi hao wananchi viwanja. Mpango wa kukamilisha viwanja 2,960. Kwa mwaka wa fedha ujao halmashauri tunakwenda kupima takribani viwanja 6,000. Viwanja hivyo, tutagawa viwanja 2,960 kwa ajili ya kukamilisha changamoto ya viwanja ambavyo wananchi wanavidai. Naamini kabisa kwa mwaka wa fedha ujao Mheshimiwa waziri tutakwenda kuondoa hiyo changamoto yote, Mungu atusaidie” alisema Kayombo.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.