Kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha taasisi na sehemu zenye mkusanyiko wa watu zaidi ya 100 kutumia nishati safi ya kupikia, imepokelewa na kufanyiwa kazi ipasavyo na uongozi wa Zabibu Hoteli, iliyopo Kata ya Tambukareli jijini Dodoma.
Hayo yamebainishwa na Meneja Mkuu wa Zabibu Hoteli, Mathew Gabriel, wakati akizungumza na vyombo vya Habari baada ya kutembelea hoteli hiyo ili kujionea matumizi ya nishati safi katika hoteli hiyo.
“Zabibu Hoteli ni miongoni mwa taasisi ambayo imejizatiti kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia kwenye kila nyanja inayohusu mapishi. Nishati safi ya kupikia ni nzuri na ina faida nyingi kulinganisha na nishati zingine zinazochangia kwenye uchafuzi wa mazingira. Kwahiyo, niziombe sekta zote na watu binafsi wajikite katika matumizi ya nishati safi za kupikia kwasababu ni rahisi na salama” alisema Gabriel.
Nae, Focus Mwenda, Mpishi Mkuu wa Zabibu Hoteli, alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuanzisha kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini. “Sisi kama Zabibu Hoteli, tunaunga mkono juhudi za Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, za kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwenye shughuli zote za mapishi. Kiukweli, nishati safi ni nzuri kwasababu inaokoa muda na ni rahisi pia kupatikana na kutumia” alisema Mwenda.
Kwa upande wake, Juma Michael, Diwani wa Kata ya Tambukareli, akatoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatumia nishati safi ili kusaidia kutunza mazingira. “Nitoe rai kwa jamii inayotuzunguka kuhakikisha inantumia nishati safi ya kupikia. Kwa sababu hii ni kampeni ya kitaifa, dhima ya Rais wetu ni kuhakikisha kila mwananchi anatumia nishati safi na salama ili mazingira ya nchi yetu yawe bora na afya za wananchi ziwe bora pia” alimalizia Michael.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.