Na. Rehema Kiyumbi, DODOMA
Afisa Kilimo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Nkunde Kimweri amesema kuwa zao la zukini ni zao lenye vitamini ambalo hutumika kama kiungo cha mboga ili kuleta ladha na kiafya hutumika kupunguza shinikizo la damu.
Alisema kuwa zao la zukini ni jepesi kupanda na lina matokeo mazuri. ’’Tulitumia mbolea na dawa kutoka Kampuni ya Fomi kuzia na baadae tukatumia Fomi nenepesha ilipoanza kutoa maua. Pia tulitumia dawa ya 40-44 kutoka Kampuni ya Jumbo kudhibiti wadudu na kuhakikisha usalama na ubora wa zao letu, lakini pia tunamshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa kutuletea vitu muhimu katika kukuza mazao yetu na hatujapata changamoto yoyote hadi hapa tulipofikia,” alisema Kimweri.
Alimalizia kwa kuwashauri vijana walio jumbani wakati wakisubiri ajira wajikite katika kilimo ili kujipatia kipato. ’’Tunawashauri vijana wachukue mikopo inayotolewa na halmashauri ili wajikite katika kilimo na kujikwamua kiuchumi katika maisha yao na kama tunavyofahamu kilimo kinamtoa kimaisha kijana kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine na hii ni kweli kupitia shuhuda tulizoziona,” alimalizia Kimweri.
Naye, Afisa Kilimo Kata ya Zuzu, Michaeli Lukumai alieleza aina ya umwagiliaji unaotumika na kuhakikisha elimu inatolewa kwa wakulima. ’’Tunatumia umwagiliaji wa njia ya matone (drip irrigation) na elimu haina mwisho tunaitoa kila siku na niendelevu ni mojawapo ya jukumu langu kama afisa kilimo kuwaelekeza wakulima wa kata yangu,” alimalizia Lukumai.
MWISHO
Imehaririwa na Nancy Kivuyo
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.