• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ziara ya Ndayishimiye, kuimarisha uhusiano Burundi na Tanzania

Imewekwa tarehe: October 22nd, 2021

RAIS wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye amewasili nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku 3 yenye lengo la kuimarisha uhusiano baina ya nchi yake na Tanzania.

Mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma, Mhe. Rais Ndayishimiye amepokelewa na mwenyeji wake Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake pamoja na kupigiwa mizinga 21.

Mhe. Rais Ndayishimiye amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Rais Samia pamoja na  kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya uhusiano na ushirikiano wa nchi hizi mbili.

Katika mazungumzo na waandishi wa habari, Mhe. Rais Samia amesema Tanzania inaridhishwa na uhusiano mzuri na wa kidugu uliopo kati yake na Burundi na kusisitiza kuwa uhusiano huo utadumishwa.

Mhe. Rais Samia amempongeza Mhe. Rais Ndayishimiye kwa jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali yake katika kuimarisha hali ya amani na utulivu pamoja na kuimarisha umoja wa kitaifa wa Warundi.

Pia, Mhe. Rais Samia amempongeza Mhe. Ndayishimiye kwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali yake katika kuimarisha uchumi ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa, kuondoa tozo kwenye sekta ya kilimo pamoja na kutoa mikopo kwa wanawake na vijana.

Aidha, Mhe. Rais Samia ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania inaungana na Burundi kulaani matukio ya kigaidi yaliyotokea tarehe 18 na 20 Septemba, 2021 nchini Burundi na kusababisha vifo vya watu 9 na wengine kujeruhiwa  pamoja na uharibifu wa mali.

Mhe. Rais Samia amesema Tanzania inaendelea na utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa wakati wa Mkutano wa Sita wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) uliofanyika Kigoma tarehe 3 hadi 5 Machi, 2021 na kuishukuru Burundi kwa hatua ya  utekelezaji wa makubaliano hayo.

Amemhakikishia Mhe. Rais Ndayishimiye kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Burundi katika kulinda na kuimarisha ulinzi hususan kwenye mipaka ya nchi hizi mbili.

Kuhusu ushirikiano katika sekta ya biashara na  Uwekezaji, Mhe. Rais Samia amesema biashara kati ya Tanzania na Burundi inaendelea kushamiri na kuongezeka.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa mualiko wa kuja kutembelea Tanzania katika ziara hiyo ambayo amesema inazidi kuimarisha uhusiano wa kidugu baina ya mataifa hayo uliokuwepo kwa muda mrefu.

Mhe. Rais Ndayishimiye amempongeza Mhe. Rais Samia kwa kuongoza nchi vizuri na kuonyesha mfano bora kwa wanawake kuwa wanaweza wanapopata nafasi.

Aidha, Mhe. Ndayishimiye ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kupitia majukwaa mbalimbali ya kimataifa kuitetea kupata haki na kuipigania kuondolewa vikwazo na Jumuiya za Kimataifa ambapo Burundi  inategemea vikwazo hivyo vitakwisha hivi karibuni.

Vilevile, Mhe. Nadyishimiye amemuhakikishia Mhe. Rais Samia kuwa kiwanda cha kuzalisha mbolea cha ITRACOM, kilichopo Nala Jijini Dodoma kitatoa ajira sawa kwa raia wa Burundi na Tanzania na kitapunguza uhaba wa mbolea hapa nchini pindi kitakapokamilika.

Pia. Mhe. Rais Ndayishimiye ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuipatia eneo kwa ajili ya ujenzi wa bandari kavu katika eneo la Kwala Ruvu mkoani Pwani na Katosho Kigoma ambazo zitasaidia kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo na kuongeza tija katika uzalishaji.

Mhe. Rais Ndayishimiye anatarajiwa kuhudhuria Dhifa ya Kitaifa leo jioni iliyoandaliwa kwa heshima yake na Mwenyeji wake Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhruri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimtambulisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye kwa Viongozi mbalimbali wa Serikali mara kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye wakati nyimbo za Mataifa mawili Tanzania na Burundi pamoja na wimbo wa Afrika Mashariki  zikipigwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na  Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba 2021.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.