• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Zoezi la ulipaji fidia kupisha ujenzi wa Reli ya SGR Morogoro - Makutupora lapamba moto Jijini Dodoma

Imewekwa tarehe: September 18th, 2020

SHIRIKA la Reli Tanzania TRC linaendelea na zoezi la ulipaji wa fidia jijini Dodoma kwa wananchi ambao maeneo yao yametwaliwa na mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR kipande cha Morogoro hadi Makutupora, hivi karibuni septemba 2020. Zoezi hili ni muendelezo wa awamu kadhaa za ulipaji wa fidia jijini Dodoma, ambapo maafisa kutoka Shirika la Reli Tanzania wapo jijini Dodoma kuhakikisha wananchi ambao maeneo yao yalitwaliwa na mradi wanapata stahiki zao kama inavyotakiwa. Pamoja na maeneo mengine ya jijini Dodoma Wananchi ambao wanalipwa fidia katika awamu hii ya zoezi la ulipaji fidia ni pamoja na wale wa maeneo ya Ihumwa, Pinda, Mkalama “A”, Miganga, Muungano “B” na Bwawani.

Mthamini kutoka Shirika la Reli Tanzania, Bi. Benlulu Lyimo, amesema kuwa katika zoezi hili la siku 10 linalotarajiwa kumalizika tarehe 20 mwezi Septemba 2020, wafidiwa kutoka mitaa 22 ya jiji la Dodoma na vijiji 9 vya wilayani Bahi wanatarajiwa kulipwa. “Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania TRC, imejipanga kulipa wafidiwa wote na tunawahakikishia kuwa kila ambae eneo lake limetwaliwa na mradi ni lazima atalipwa stahiki zake” aliongeza Bi. Lyimo. Zoezi hili la ulipaji fidia linaenda sambamba na kuwashauri wafidiwa juu ya namna bora ya matumizi ya fedha hizo ili kuwaletea wananchi hao maendeleo.

Aidha, msimamizi wa masuala ya kijamii, Bi. Catherine Mwakigali amesema kuwa “kuna wengine wanafikiria kufanyia starehe, kwa hiyo tunawashauri kuzitumia vizuri pesa hizo ikiwemo kwenda kuanzisha makazi mapya au shughuli nyingine za kimaendeleo kama vile biashara”

Kwa upande wake mmoja wa wananchi waliolipwa fidia zao, Bwana Hamisi Samson amesema “kwa kutumia fedha hizi nitajenga nyumba nyingine, nitasomesha watoto na shughuli nyingine za kimaendeleo”

Zoezi hili ni utekelezaji wa ahadi ya kuwa kila mwananchi ambae eneo lake limetwaliwa na mradi, atalipwa na mpaka sasa ujenzi wa reli ya kisasa SGR katika kipande cha Morogoro - Makutupora, umefikia zaidi ya 35%.

Chanzo: tzrailways (instagram)

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.