MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango leo ametembelea mitaa mbalimbali ya Jiji la Dodoma ikiwemo Soko Kuu la Majengo kukagua utunzaji wa mazingira katika maeneo hayo.
Mhe. Mpango ameagiza kuwa zoezi la usafi ni muhimu likawa endelevu kwa nchi nzima na viongozi wanapaswa kulisimamia.
Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Mpango aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthon Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweli, Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru na viongozi mbalimbali.
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Mstahiki Meya wa Jjiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe alipotembelea Soko Kuu la Majengo kukagua utunzaji wa mazingira.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.