• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mkataba wa ununuzi wa behewa 1430 za mizigo za reli ya kisasa – SGR wasainiwa

Imewekwa tarehe: February 8th, 2022

Shirika la Reli Tanzania – TRC limesaini mkataba na kampuni ya CRRC International kutoka nchini China kwa ajili ya ununuzi wa Behewa 1430 za mizigo zitakazotumika katika reli ya kisasa – SGR, hafla ya utiaji saini imefanyika katika ukumbi wa mikutano makao makuu TRC Februari 08, 2022.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali na Shirika, ambapo Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TRC, Mkurugenzi Mkuu TRC, Wawakilishi wa kampuni ya CRRC International, Menejimenti na Wafanyakazi wa TRC pamoja na wanahabari.

Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ameshuhudia zoezi la utiaji saini mara baada ya kupata taarifa fupi ya mkataba wa ununuzi wa behewa hizo pamoja na maendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa nchini kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa kuwa Ujenzi wa reli ya kisasa unaoendelea kwa sasa ni kipande cha Dar es Salaam – Morogoro umefika 95%, Morogoro – Makutupora umefika 81% na Mwanza – Isaka umefika 4%.

Hata hivyo Waziri Mbarawa alisema kuwa katika Behewa hizo 1430 zitakazotengenezwa zipo Behewa 60 za mifugo ambapo Behewa moja itakuwa na uwezo wa kubeba takribani Ngo’mbe 100 ambayo ni sawa na Ngo’mbe 6,000 kwa behewa 60. Pia zipo behewa 50 maalumu kwa ajili ya kubeba magari ambapo behewa moja itakuwa na uwezo wa kubeba magari madogo 8 ambayo ni sawa na magari 400 kwa behewa 50.

Mhe. Waziri alifafanua kuwa “kutokana na uwezo mkubwa wa reli ya kisasa, behewa hizi zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza mrundikano wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam ambapo treni moja itakuwa na uwezo wa kubeba Tani 10,000 kwa mkupuo ambayo ni sawa na malori 500” alisema Prof. Mbarawa.

Katika hatua nyingine, Mhe. Waziri aliwapongeza wafanyakazi wa Shirika la Reli kwa usimamizi mzuri wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa na kuwaomba waendelee kuchapa kazi kwa kutumia weledi walionao na jitihada ili kutimiza malengo ya Serikali ya kuhudumia wananchi na kukuza uchumi wa Taifa.

Mkurugenzi Mkuu TRC, Ndugu Masanja Kadogosa katika taarifa yake amesema kuwa,
“Mkataba huu ni wa ununuzi wa behewa 1430 za mizigo za reli ya kisasa ambao unagharimu Dola za Kimarekani Milioni 127.2, ni mkataba wa miezi 12 yaani mwaka mmoja utakaohusisha usanifu na utengenezaji wa behewa kwa ajili ya kubeba mizigo ya aina mbalimbali kulingana na aina ya behewa na matakwa ya mteja kupitia reli ya kisasa”.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi mkuu aliweka wazi kuwa aina ya behewa zitakazonunuliwa kupitia mkataba huu ni, behewa 600 aina CCB (Container Carrier Bogie) kwa ajili ya kubeba makasha, behewa 400 aina ya CLB (Covered Large Bogie) kwa ajili ya kubeba mizigo ya jumla ikiwemo Sukari, Saruji, Chumvi, Pamba, Tumbaku na Kahawa, behewa 190 aina ya PTB (Petroleum Tank Bogie) kwa ajili ya kubeba mafuta aina zote, Behewa 70 aina ya HLB (High Large Bogie) kwa ajili ya Mabomba, Mbao, Magogo na Vyuma, behewa 50 aina ya MGB (Motor Goods Bogie) kwa ajili ya kubeba magari na behewa 50 aina ya CWB (Cattle Wagon Bogie) kwa ajili ya kubeba Ng’ombe.

Kwa upande wake Mwakilishi wa kampuni ya CRRC ambaye ni Meneja Msaidizi Bw. Tang Yun Peng amesema kuwa “Leo ni siku nzuri kwetu CRRC kwa sababu haikuwa rahisi kufikia hapa, nakumbuka mwaka jana tulishiriki katika mradi wa uboreshaji wa reli ya kati, hivyo tuna ujasiri wa kutosha kusanifu na kutengeneza behewa bora na imara kwa ajili yenu” alisema Bw. Peng.

Shirika la Reli Tanzania linatarajia kukamilika kwa manunuzi na kuwasili kwa behewa hayo mapema Februari 2023 ambako kutakwenda sambamba na kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha pili Morogoro – Makutupora ambacho kwa umbali huo kutaweza kuleta tija na faida katika uendeshaji wa huduma ya usafirishaji mizigo.

Chanzo: Tovuti ya TRC

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma atoa pongezi kwa Madiwani

    May 25, 2025
  • Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

    May 23, 2025
  • Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

    May 23, 2025
  • Wananchi Kata ya Madukani washukuru kuboreshwa huduma za Afya, Zahanati ya Chikande

    May 21, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.