Huduma za afya:
Halmashauri ya Jiji la Dodoma inatoa huduma mbalimbali wa wakazi wa manispaa na wananchi kutoka nje ya Jiji. Jiji lina Vituo vya Afya 4 na zahanati 32.
Katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuna hospitali 4, kati ya hizo 2 zinamilikiwa na Serikali na 2 zinamilikiwa na taasisi za kidini. Kuna jumla ya vituo vya afya 13, kati ya hivyo 4 vinamilikiwa na Halmashauri, 4 na taasisi za serikali, 3 na taasisi za kidini na 2 ni vya binafsi.
Hata hivyo, kuna zahanati 48, kati ya hizo 32 ni za serikali, 6 ni za taasisi za kidini, 2 zinamilikiwa na taasisi za serikali na 8 za watu binafsi. Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General Hospital) inatumika kama na wakazi wengi wa jiji kwa kuwa Halmashauri bado haina hospitali yake ya Wilaya; hii imesababisha msongamano mkubwa wa wagonjwa katika hospitali ya mkoa. Juhudi zinafanyika ili kujenga hospitali ya Wilaya.
Kwa sasa Halmashauri imeingia mkataba wa huduma na Hospitali ya Mt. Gemma kufanya kazi kama Hospitali teule ya Wilaya wakati juhudi za kujenga Hospitali ya Wilaya zinaendelea.
Kuhusiana na suala la afya, Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina magonjwa 10 ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara, kama inavyoorodheshwa hapa chini:-
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.