MIAKA 23 BILA MWALIMU J.K. NYERERE, NAIKUMBUKA KAULI YA 'MTU NI AFYA'
Na Abdallah Mahia
Naikumbuka kaulimbiu ya ‘Mtu ni Afya’. Mtu ni Afya ya Mwalimu Nyerere ni kielelezo juu ya Afya Mazingira. Serikali ya awamu ya kwanza ilijali sana shughuli za Afya Mazingira sambamba na usemi wa ‘kinga ni bora kuliko tiba’.
Watanzania wanapokumbuka Mwalimu Nyerere pia wanaikumbuka sana kaulimbiu ya ‘Mtu ni Afya’ ambayo iliimbwa sana magazetini, redioni, sehemu za mikusanyiko ikiwemo mikutano mbalimbali.
‘Mtu ni Afya’ ilisaidia kuwahamasisha wananchi juu ya kujikinga na adui maradhi. Hii ni kauli iliyoletwa na Serikali ya Mwalimu J.K. Nyerere mwaka 1973-78. Katika kuendeleza kumuenzi Mwalimu Julius K. Nyerere zaidi tujikumbushe mikakati iliyowekwa katika njia ya ‘Mtu ni Afya’ tuuige na tuweke katika njia tulizonazo.
Tuendeleze kuongeza jitihada kubwa kwa kuhakikisha tunazuia kuongezeka kwa magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa kufanya usafi wa mazingira pamoja na kuijali kinga na kuona umuhimu wake kwani tukifanya hivyo tunapunguza umasikini tukizingatia kwamba gharama za matibabu ni kubwa kuliko gharama za kinga.
Tukumbuke kuweka Mipango yetu ya bajeti ya kutosha katika shughuli za kujikinga ili kuenzi sera tukuka ya ‘Mtu ni Afya’ iliyotokana na fikra sahihi za Mwalimu Julius K. Nyerere.
‘Mtu ni Afya’ ililenga kutoa ujumbe maalum kwa jamii kwamba bila mazingira safi binadamu hawezi kupata afya bora, na anakuwa muhanga wa maradhi yote hatari. Tunapomkumbuka Mwalimu Julius K. Nyerere tunaikumbuka kauli mbiu ya ‘Mtu ni Afya,’ jali usafi wa mazingira kwani ‘Mtu ni Afya’.
Abdallah Mahia ni Afisa Afya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Makala za nyuma:
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.