Kufungwa kwa shule kwa muda mrefu kulikolenga kuwaweka wanafunzi kuwa salama dhidi ya COVID-19, kumeanza kunawaumiza kwa upande mwingine, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na UNICEF yamesema, yakihimiza serikali barani Afrika kuzifungua tena shule huku wakichukua tahadhari kuwakinga na kuenea kwa virusi.
Katika Utafiti uliofanywa na WHO katika nchi 39 za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara umegundua kuwa nchi sita tu (ikiwemo Tanzania) ndizo zilizofungua shule. Nchi 14 shule zimefungwa na nchi 19 zinafungua kwa dharura (madarasa ya mitihani). Hata hivyo nchi kadhaa zimepanga kuanza masomo mnamo mwezi Septemba, ambapo ni mwanzo wa mwaka wa masomo katika baadhi ya nchi.
Mashirika hayo yamesema kuendelea kufunga shule kwa muda mrefu kunahatarisha ustawi wa watoto hao ikiwa ni pamoja na lishe duni, kuongezeka kwa uwezekano wa vurugu na udhalilishaji, mimba za utotoni na changamoto za jumla katika ukuzaji wa akili kwa watoto.
Katika Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, UNICEF imegundua viwango vya ukatili dhidi ya watoto viko juu, wakati viwango vya lishe viko chini kwa zaidi ya watoto milioni 10 kukosa chakula cha shule. Kwa wasichana, haswa wale ambao wametengwa au wanaishi katika kaya zenye kipato cha chini, hatari ni kubwa zaidi. Kwa mfano, kufuatia kufungwa kwa shule kuliyosababishwa na mlipuko wa Ebola huko Afrika Magharibi mwaka 2014, viwango vya ujauzito kwa vijana nchini Sierra Leone viliongezeka mara mbili na wasichana wengi hawakuweza kuendelea na masomo mara shule zilipofunguliwa tena.
Athari ya muda mrefu ya kijamii na kiuchumi kutokana na kufungwa kwa muda mrefu ni jambo la kulitilia maanani. Kulingana na mfano wa Benki ya Dunia, kufungwa kwa shule katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kunaweza kusababisha kupungua kwa kipato kiasi cha dola za Kimarekani 4500 kwa kila mtoto. Hii inaweza kuzidishwa pia na kipato kidogo cha wazazi wanaolazimika kukaa nyumbani ili kutunza watoto haswa katika kaya ambazo haziwezi kumudu huduma za matunzo ya watoto.
"Shule zimeweka njia ya kufanikiwa kwa Waafrika wengi. Pia zinatoa nafasi salama kwa watoto wengi katika mazingira magumu ya kukuza na kufanikiwa" alisema Dk Matshidiso Moeti (pichani juu), Mkurugenzi Mkuu wa WHO wa Kanda wa WHO. "Lazima tusiwe vipofu na juhudi zetu za kuwa na COVID-19 na kuishia kupoteza kizazi chetu. Kama nchi zimeweza kufungua biashara kwa usalama, basi tunaweza kufungua shule pia. Uamuzi huu lazima uongozwe na uchambuzi wa vihatarishi ili kuhakikisha usalama wa watoto, waalimu na wazazi na kwa hatua muhimu kama kukaa umbali unaokubalika” alisisitiza Moeti.
WHO, UNICEF na Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu wametoa mwongozo wa kuzuia na kudhibiti COVID-19 mashuleni. Mwongozo huo unamapendekezo ya umbali wa kutumika kati ya mtu na mtu, kuzuia hafla za shule zenye msongamano wa watu, kuweka nafasi kati ya madawati, kutoa vifaa vya kunawia mikono, kuvaa masks, kuzuia kugusana kusiko kwa lazima na kuhakikisha kuwa wanafunzi na waalimu wagonjwa wanabaki nyumbani.
Dr Moeti na Bwana Fall walifanya mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na APO Group jana tarehe 21/08/2020
Chanzo: www.unicef.org
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.