MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA ANAWATANGAZIA WAKAZI, WAFANYABIASHARA, NA TAASISI ZOTE ZILIZOKO KATIKA JIJI LA DODOMA KUWA MWISHO WA MATUMISI YA MIFUKO YA PLASTIKI NI TAREHE 31/05/2019.
IFIKAPO TAREHE 01/06/2019 HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA KWA YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUZALISHA, KUINGIZA, KUSAMBAZA, KUUZA NA KUTUMIA MIFUKO YA PLASTIKI NDANI YA JIJI LA DODOMA.
EWE MWANANCHI NA MFANYABIASHARA CHUKUA HATUA SASA ACHANA NA MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI NA TUMIA MIFUKO MBADALA.
KUMBUKA MIFUKO YA PLASTIKI INA ATHARI KWA AFYA NA MAZINGIRA.
KWA WAFANYABIASHARA WOTE WATAKAOKUWA NA AKIBA YA MIFUKO HIYO BAADA YA TAREHE 31/05/2019 WAISALIMISHE KATIKA OFISI ZA MITAA NA KATA ZILIZOPO KARIBU YAO.
USOMAPO TANGAZO HILI, TAFADHALI MTAALIFU NA MWENZAKO
Imetolewa na:
MKURUGENZI WA JIJI
HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.