.Na. Sizah Kangalawe
Habari Dodoma Rs
Wadau wa sekta ya Afya wamepongezwa kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kutokomeza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua na watoto wa umri chini ya Miaka 5.
Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Septemba 26 Mwaka huu wakati alipotembelea kituo cha afya Ugogoni, Wilayani Kongwa ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi Wilayani humo.
"Niwashukuru wadau ambao wameona sababu ya kushirikiana na Serikali yetu katika kukamilisha eneo hili la kimkakati ambalo linaendana na maono ya Serikali na miongozo yetu. Nchi yetu imekua ikipambana sana kupunguza vifo vya kina mama na watoto.
Hapa naambiwa mama ambaye bahati mbaya mtoto amefariki akiwa tumboni atapata huduma hiyo ambayo isipotolewa kwa umakini inaleta hatari kwa mama, angalau hapa patasaidia kufanya mama huyo apate mazingira rafiki ya kuokoa uhai wake", amepongeza Mhe. Senyamule
Kituo cha Afya Ugogoni kilipokea fedha kiasi cha Tsh. 23,380,000/= kutoka kwa wadau wa BUFFET FOUNDATION kwaajili ya ujenzi wa jengo maalumu la huduma ya dharura itolewayo kwa ujauzito ulioharibika.
Akizungumza katika eneo la ujenzi wa kituo cha Afya Laikala, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka S. Mayeka amepongeza juhudi za Serikali ya awamu ya 6 katika sekta ya Afya.
"Kituo hiki cha afya Laikala kitakuwa ni kituo cha 10 kwenye Wilaya yetu na Katika vituo 10 tulivyonavyo, vituo 6 vimejengwa ndani ya Miaka 4 ya Serikali ya awamu ya sita, kwahiyo unaweza kuona Rais wetu anavyofanya kazi kwa bidii ya kuleta maendeleo", alisema Mhe. Mayeka
Katika ziara hiyo RC Senyamule alitembelea na kukagua Miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Bweni la Shule ya Sekondari Kimaghai A' na Ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa pia ujenzi wa madarasa 2 na matundu ya vyoo katika Shule ya msingi Kongwa, ujenzi wa jengo la dharula Kwa wajawazito la kituo cha afya Ugogoni na Ujenzi wa kituo cha afya Laikala.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.