Na. Hellen M. Minja
Habari – DODOMA RS
Viongozi wa Klabu ya Michezo ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Mwenyekiti wake Dr. Nassoro A. Matuzya, wamefanya mazungumzo mafupi na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma juu ya ushiriki wao kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) 2025.
Sambamba nae, pia ameongozana na Viongozi wengine ambao ni Katibu wa Klabu Bw. Majuto Msekela, Nahodha wa Timu ya Michezo ya Wanaume Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. Prosper Sanga na Mjumbe wa Kamati ya Michezo ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Bw. John Kidasi kwenye Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa Jengo la Mkapa Jijini humu.
Lengo la mazungumzo hayo ni kumpatia taarifa ya ushiriki wao katika Mashindano hayo ambayo mwaka huu, yamefanyika Mkoani Mwanza, huku timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ikifanikiwa kushiriki michezo hiyo kwa kupeleka Timu ya Wanaume ambayo iliwakilisha katika michezo ya Mpira wa Miguu na kufika hatua ya16 bora.
Aidha, Mchezo mwingine ambao Timu hiyo ilishiriki ni wa kusukuma kete (Draft) kwa Wanaume ambapo walifanikiwa kufikia hatua ya robo fainali na Timu kukabidhiwa Cheti, Medali ya ushiriki sambamba na Jarida la taarifa ya Shirikisho hilo kwa mwaka uliopita wa 2024.
Hata hivyo, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Khatibu Kazungu, ametoa rai kwa Viongozi hao kujiandaa vizuri na mapema kwa ajili ya mashindano ya mwakani kwa kuhakikisha wanapeleka timu yenye uwezo thabiti wa kurudi na ushindi kwa sababu Mkoa una Watumishi wa kutosha na wenye uwezo wa kushiriki mashindano hayo ipasavyo.
Michezo ya SHIMIWI ni maelekezo ya Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan - aliyoyatoa Agosti 14, 2025 kwa kuelekeza Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kuhakikisha Wizara, Taasisi na Idara zote za Serikali zinashiriki na mwaka huu
ilianza Septemba Mosi na kuhitimishwa Septemba 16 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.