Na Sofia Remmi.
Habari - Dodoma RS
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amesema kukosekana kwa hoteli zenye hadhi ya nyota tano kumekuwa kikwazo kwa mikutano mikubwa ya kimataifa kufanyika katika Mkoa huu, licha ya uwepo wa makao makuu ya Serikali.
Mhe. Senyamule amesema hayo tarehe 30/09/2025 alipokuwa akizungumza na wamiliki wa hoteli wa Mkoa wa Dodoma.
Amesema kutokana na hali hiyo sekta binafsi inalo jukumu la kuhakikisha kuwa unafanyika uwekezaji utakaokidhi mahitaji hayo.
"Hivi sasa hatuna hoteli zenye hadhi ya nyota tano ambazo zingeweza kutumiwa na wageni wa kimataifa ambao wanakuja Nchini kwa ajili ya shughuli mbalimbali.
Amesema, viwango vya kimataifa vinahitaji uwepo wa hoteli zenye hadhi ya nyota tano zisizopungua tano ndipo kuwa na uwezo wa kufanyika kwa shughuli hizo katika eneo husika hivyo kutoa wito kwa wawekezaji kutumia fursa hiyo.
"Nitoe wito kwa wawekezaji kuwekeza hoteli zenye hadhi ya nyota tano au mziboreshe zilizopo hivi sasa ili ziweze kufikia hadhi hiyo, serikali imefanya uwekezaji mkubwa sana ikiwamo ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa Msalato.
"Mikutano mikubwa ya kimataifa huwa inafanyika katika makao makuu ya nchi, lakini hivi sasa hatuwezi kutokana na kukosa hoteli na kumbi kubwa zenye hadhi, hivyo hatuna budi kuwekeza katika sekta hii muhimu, "amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wamiliki wa Hotel Mkoa wa Dodoma Bw.Gabriel Mauna amezipongeza mamlaka za maji na Umeme kwa kufanya maboresho katika sekta zao na kusababisha kurahisishwa kwa huduma hizo muhimu.
“Tunashukuru Serikali ya Mkoa, kwasababu mara ya mwisho tulipokutana, tulitoa changamoto zetu na mojawapo ilikuwa ni umeme na maji, tunashukuru changamoto hizi zimefanyiwa kazi na katika hili nawapongeza DUWASA na TANESCO kwa kuboresha huduma hizi za muhimu kwetu", amesema Mauna
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.