Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) ina jukumu la kuratibu na kusimamia Uchaguzi waSerikali za Mitaa wa mwaka 2019, kwa kushirikiana na wadaumbalimbali wa Uchaguzi. Katika kutekeleza jukumu hilo, OR-TAMISEMI imeandaa Miongozo mbalimbali ukiwemo Mwongozo huu wa Elimu ya Mpiga Kura utakaotumiwa na wadau wote wa Uchaguzi katika kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi.
Lengo la elimu ya mpiga kura ni kuwahamasisha na kuwawezesha wananchi na wadau wa Uchaguzi kuelewa mchakato wote wa Uchaguzi, kanuni na taratibu muhimu za Serikali za Mitaa ili waweze kushiriki na kutumia haki yao ya Kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi za uongozi wa Serikali za Mitaa.
Elimu ya Mpiga Kura itawawezesha wananchi kutambua haki na wajibu wao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili waweze kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi huo.
Kupakua na kusoma Mwongozo huu bofya hapa:- MWONGOZO WA ELIMU YA MPIGA KURA.pdf
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.