Kuanzia leo Alhamisi Machi 29, 2018 njia za Daladala Manispaa ya Dodoma zimebadilika kwa kurefushwa pamoja na kufuta Standi ya Jamatini, badala yake zitatakiwa kuishia Nanenane standi mpya ya mabasi.
Ofisa Mfawidhi Kanda ya Kati wa Sumatra, Conrad Shiyo amesema. Njia hizi ndefu zimepangwa kwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi, Manispaa ya Dodoma, na Chama cha Wamiliki wa Daladala (UWEDO).
UDOM - VEYULA
Katika marekebisho hayo, daladala zinazofanya kazi kati ya UDOM na Veyula zitakuwa zikitoka UDOM zinapita kwa Waziri Mkuu, Posta, Hospitali ya General, Independence, Sango na kupita NBC na kwenda Veyula, na wakati wa kurudi kutoka Veyula zitapita Paradise, Nyerere, Posta hadi UDOM.
NALA - BENJAMIN MKAPA HOSPITAL
Daladala kutoka Nala zitapita Sango, Hospitali ya Mkoa, Posta hadi hospitali ya Benjamin Mkapa na kurudi kupitia Posta, Hospitali ya Mkoa, Independence hadi Nala.
VEYULA - NANENANE
Kutakuwa na njia ya Veyula hadi Nanenane, daladala zake zitapita Paradise, Nyerere, CBE hadi Nanenane na kurudi kupitia CBE. Carnical, General, Independence, Sango, NBC na kurudi Veyula.
CHANG'OMBE - NANENANE
Daladala kutoka Chang'ombe hadi Nanenane, zitapita Paradise, Nyerere, CBE hadi Nanenane na wakati wa kurudi zitapita CBE, Carnival, General Hospital, Independence, Sango na kurudi Chang'ombe.
ST. GEMA - SWASWA/NANENANE
Magari kutoka St Gema hadi Swaswa au Nanenane, yatapita Paradise, Nyerere, CBE hadi Swaswa na Nanenane na kutoka huko Nanenane zitapita CBE, Carnival, General, Independence, Sango, NBC na kurudi St Gema.
NKUHUNGU - NANENANE
Daladala za Nkuhungu zitapita vituo vya Sango, General, CBE, hadi Nanenane na kurudi kwa kupitia kituo cha CBE, Carnival, Independence, Sango hadi Nkuhungu.
MKONZE - NANENANE
Daladala kutoka Mkonze zitapita vituo vya Kikuyu, Majengo, General, CBE hadi Nanenane na wakati wa kurudi zitapita CBE, Carnival, General, Majengo, Kikuyu hadi Mkonze.
SWASWA, UZUNGUNI NA NANENANE
Daladala za kutoka Swaswa, Uzunguni na Nanenane na kurudi zitapitia vituo vya CBE, Carnival kisha njia ya uelekeo wa baabara ya Sabasaba hadi D-Center (Makole) kisha kutokea mbele ya CBE na kurudi yalikotokea.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.