Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma anawatangazia wananchi wote kuwa na Tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Corona (COVID-19)
Ugonjwa huu husambaa kwa njia ya hewa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine kupitia vitone vidogo vidogo vya mate vinavyoruka toka puani au mdomoni kutoka kwa mtu mwenye maambukizi ya virusi hivyo anapopiga chafya, kukohoa au kupumua au kwa kugusa majimaji au makamasi kutoka kwa mgonjwa.
Dalili huanza kuonekana kati ya siku moja hadi kumi na nne(1-14) tangu kupata maambukizi.
Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na
Mtu huweza kujikinga kwa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia dawa maalumu ya kuua wadudu (Hand sanitizer);
Baada ya kushika kinyesi cha mnyama au mnyama mwenyewe
Kwa sababu
Ukinawa mikono kwa sabuni na maji au kutumia dawa maalumu ya kusafisha mikono utaua virusi ambao hukaa kwenye mikono .
Jiweke mbali zaidi ya mita moja kutoka kwa mtu anayekohoa au kupiga chafya.
Kwa sababu
Mtu anapopiga chafya au kukohoa hurusha chembechembe za mate ambazo huweza kuwa zimebeba virusi. Ukiwa karibu sana utawavuta virusi hawa unapovuta hewa.
Zingatia kanuni za afya na usafi ikiwa ni pamoja na kukaa mbali na mtu mwenye dalili za mafua mwenye historia ya kusafiri katika nchi zilizokumbwa na ugonjwa huu.
Funika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kitambaa safi.
Epuka kugusana na mgonjwa mwenye dalili za magonjwa ya njia ya hewa
Epuka kushikana mikono/kukumbatiana au kupigana busu .
Tangazo hili limetolewa na mkurugenzi wa Jiji la Dodoma
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.