TANGAZO
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA KWA MARA NYINGINE ANAWATANGAZIA WAFANYABIASHARA WOTE WANAOFANYIA BIASHARA ZAO KWENYE VIBANDA NDANI YA SOKO LA SABASABA, BONANZA, KIKUYU KUSINI, CHANG’OMBE NA MAJENGO KUWA MNATAKIWA KUANZA KULIPIA MIKATABA PAMOJA NA PANGO LA VIBANDA HIVYO.
TAFADHARI FIKA KATIKA OFISI YA MTENDAJI WA KATA LILIPO SOKO UNALOFANYIA BIASHARA ILI KULIPIA MIKATABA NA PANGO LA KIBANDA UNACHOFANYIA BIASHARA KABLA YA TAREHE 25/10/2021.
KUANZIA TAREHE 30/10/2021 UKAGUZI UTAANZA RASMI KUBAINI VIBANDA AMBAVYO HAVIJALIPIWA NA HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA IKIWA NI PAMOJA NA KUVIFUNGIA VIBANDA HIVYO.
TIMIZA WAJIBU BILA SHURUTI
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA
MKURUGENZI WA JIJI LA DODOMA
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.