Msimamizi wa Uchagui wa Jiji la Dodoma anawataarifu wananchi wote kuwa, kuanzia tarehe 22 Oktoba, 2019 ndio ukomo wa kuwa madarakani kwa Wenyeviti na Wajumbe wa Mtaa ndani ya Jiji la Dodoma.
Hivyo basi, wananchi mnajulishwa kuwa hakutakuwa na nyaraka yo yote au huduma yo yote itakayotambuliwa kisheria ikiwa imetolewa na Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Mtaa kuanzia tarehe 22 Oktoba, 2019.
Huduma zote zitaendelea kutolewa na Watendaji wa Mitaa/Kata husika hadi pale Uchaguzi wa Viongozi utakapokamilika tarehe 24 Novemba, 2019.
Kwa maelezo zaidi bofya hapa: Tangazo la Ukomo wa Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za Mitaa
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.