Wednesday 22nd, January 2025
@Nyerere Square
Halmashauri ya Jiji la Dodoma itatoa mikopo kwa wajasiliamali kwa vikundi vya akinamama, vijana na watu wenye ulemavu, mikopo inayotokana na fedha za asilimia 10 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana Sharifa Nabalang'anya alipokuwa akiongelea kuhusu maandalizi ya tukio hilo muhimu.
Sharifa amesema katika tukio hilo ambalo mgeni rasmi atakuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Joseph Mafuru, vikundi vipatavyo 14 vitapata mikopo kwa ajili ya kununulia Bodaboda, Bajaji na pia kwa ajili ya miradi ya machinjio ya kuku, salon na bidhaa za ngozi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.