Na. Hellen M. Minja
Habari – DODOMA RS
Mwenyekiti wa Baraza la kumshauri Rais kuhusu masuala ya Chakula na Kilimo nchini Tanzania ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, amewaasa wafugaji kufuga kwa kuzingatia uwezo wa malisho ili kupata tija ya ufugaji ikiwa ni pamoja na kupata maziwa na mazao mengine ya ufugaji.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti huyo alipokua akifungua Mkutano wa Wadau wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Kanda ya Kati uliofanyika Agosti 13, 2025 katika ukumbi wa Hoteli ya Morena Jijini Dodoma ambapo mbali na ufugaji wenye kuzingatia eneo la malisho, amesema Tanzania ina eneo la hekari Milioni 44 kwa ajili ya kilimo na kwenye eneo hilo ni 15% ndio inafaa kwa kilimo.
“Fuga kulingana na eneo la malisho ili uweze kupata Ng’ombe wenye sifa na wanaosimamiwa vizuri. Tuna hekta zenye kufaa kwa kilimo Milioni 44 katika eneo hilo lote, eneo la ardhi linalolimwa ni 15% na Sekta za kilimo, Uvuvi na Ufugaji zimechangia kutoa ajira kwa wananchi asilimia 65 mpaka 70”. Mhe. Pinda
Aidha, Katibu wa Baraza hilo Dr. Florence Turuka amesema katika Mikutano ya viongozi wa nchi za Afrika, Serikali ziliazimia kuwa Afrika itumie fursa zilizopo katika kilimo na ichangie kulisha watu Bilioni 9 watakao kuwepo hapa ulimwenguni ifikapo mwaka 2050 ambapo Waafrika watakua wamefikia takribani watu Bilioni 2.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amempongeza Mhe. Rais kupitia Wizara ya kilimo kwa kuwekeza kwenye miundombinu ya kilimo na kuufanya Mkoa huu kuwa sehemu ya uzalishaji wa chakula nchini kwani ameanzisha miradi ya uchimbaji visima kwenye kila Wilaya ili kuwezesha kilimo cha umwagiliaji.
Akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi ya mwaka 2024, Katibu Tawala Msaidizi Seksheni za Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dodoma Bi. Aziza Mumba amesema sekta za Mazao, Mifugo, Uvuvi na Misitu zinachangia takribani 39% ya Pato la Mkoa na kusababisha soko kuongezeka hivyo pia uzalishaji unatakiwa kuongezeka.
Baraza la kumshauri Rais kuhusu masuala ya Chakula na Kilimo lilianzishwa Machi 14, 2023 na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuimarisha usalama wa chakul
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.