Na. Elizabeth S. Dai
Habari- DODOMA RS
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma wameelezwa juu ya fursa za kibiashara zinazopatikana katika nchi ya Indonesia.
Hayo yamebainishwa na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Tri Yogo Jatmiko leo Agosti 15, 2025 wakati akifanya mazungumzo na wafanyabiashara hao kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
“Mimi kama balozi wajibu wangu ni kuweka sawa miundombinu rafiki kwa ajili ya wafanyabiashara na kufanya mikataba ya kibiashara kati ya pande zote mbili kwenye kilimo, elimu, afya, dawa na hospitali.”amesema balozi,Mhe. Jatmiko
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe. Alhaj Jabir Mussa Shekimweri amewataka Wafanyabiashara kuchangamkia fursa walizoelezwa na Balozi huyo kuzifanyia kazi kwa kuzingatia aina za biashara.
Nae Mwenyekiti wa Baraza la biashara Mkoa wa Dodoma Bw. Vivian Komu ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwapambania Wafanyabiashara katika kukuza biashara zao Kimataifa, huku akiahidi kushirikiana na Wafanyabiashara wenzake kufanyia kazi fursa hizo.
Katika hatua nyingine, Wafanyabiashara wamekaribishwa kushiriki kwenye maonesho ya 40 ya biashara nchini Indonesia yanayokutanisha wafanyabiashara mbalimbali Kimataifa (40th Trade Expo Indonesia).
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.