Na. Hellen M. Minja
Habari - DODOMA RS
Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwl. Vicent Kayombo ametembelea na kukagua maandalizi ya Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Agosti 15, 2025.
Maadhimisho hayo ambayo ni ya Kimkoa, yanatarajiwa kufanyika Wilayani Kondoa siku ya Jumatatu Agosti 18, 2025 yakihudhiriwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.
Miongoni mwa maeneo aliyoyatembelea ni pamoja na eneo la maadhimisho, maandalizi ya maonesho yanayofanyika katika shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa na Shule ya msingi Mpalangwi pamoja na mradi wa IPOSA unaolenga kuwakomboa vijana hasa wa kike kiuchumi kwa kujifunza ujasiriamali.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.