Wednesday 22nd, January 2025
@Chuo cha Mipango
Kikao cha Baraza la Mawdiwani (Full Council) wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kinatarajia kufanyika kwa siku mbili ambapo kitaanza Aprili 25 na kuendelea Aprili 27 mwaka huu.
Kikao hicho ni cha kawaida cha Kisheria kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa mbalimbali za Maendeleo zilizotekelezwa na Manispaa katika kipindi cha cha robo ya pili mwka wa fedha 2017/8. Kipindi hicho ni katika Mwezi Januari hadi Machi, 2018.
Kwa mujibu wa utaratibu, kikao kitaanza saa 10:00 asubuhi na kuendelea hadi majira ya saa 3:00 Alasiri, katika ukumbi wa Chuo cha Mipango.
Mkurugenzi wa Manispaa anakukaribisha wewe Mwananchi na Mkazi wa Dodoma uhudhuruie ili ujue mambo ya Kimaendele yanayotekelezwa katika eneo lako na Manispaa kwa ujumla.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.