Sunday 22nd, December 2024
@Nyerere Square
Siku ya Jumamosi ya tarehe 11 Mei, 2019 kutakuwa na maadhimisho ya kitaifa ya siku ya pumu duniani kwa kufanya matembezi ya hiari kutoka viwanja vya shule ya Sekondari Dodoma hadi Nyerere Square. Mgeni rasmi wa maadhimisho haya atakuwa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo na ataambatana na baadhi ya wabunge akiwamo Mhe. Anthony Mavunde.
Maadhimisho haya yanafanywa na chama cha magonjwa ya hewa na mapafu kwa kushirikiana na Idara za Afya, Elimu Msingi na Elimu Sekondari.
Aidha, shughuli shughuli ambazo zimekwishafanyika kuelekea kilele cha maadhimisho hayo ni pamoja na kuwajengea uwezo walimu wa Afya, wanafunzi wenye pumu pamoja na baadhi ya Vituo vya tiba, sambamba na kufanya screening kwa wanafunzi ili kuwabaini na kuwapa matibabu wenye pumu mapema.
Unaalikwa kushiriki maadhimisho haya ambapo utatakiwa kufika saa moja asubuhi viwanja vya Shule ya Sekondari Dodoma na tutatembea kwa miguu hadi Nyerere Square na ratiba inatarajiwa kuisha saa nne asubuhi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.