Sunday 22nd, December 2024
@Ofisi ya Rais TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo (Mb) atafanya mkutano wa kazi na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa yote 26 ya Tanzania bara na wadau wengine.
Lengo la Mkutano huo ni kutoa Tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2019 na maelekezo mbalimbali kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Mkutano huu utarushwa moja kwa moja (live) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Wananchi wote wanakaribishwa kuangalia matangazo hayo ya moja kwa moja (mubashara) kwa njia ya runinga ili kupata taarifa muhimu kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2019.
Kwa ziada bofya hapa: Taarifa kwa Umma
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.