Wednesday 22nd, January 2025
@Soko la Majengo
Siku ya Kunawa Mikono Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 15 mwezi wa Oktoba, na katika maadhimisho ya mwaka huu jijini Dodoma, yatafanyika katika Soko la Majengo.
Hayo yamesemwa na Afisa Afya wa Jiji la Dodoma, Abdallah Mahia alipokuwa akielezea kuwa maandalizi ya maadhimisho hayo yamekwisha kamilika na kwamba ratiba itaanza saa 3 asubuhi sokoni Majengo ambapo mgeni rasmi atakuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru.
Mahia amewakaribisha wananchi wote kufika na kusikia ujumbe wa maadhimisho hayo yanayolenga kuwakumbusha wananchi juu ya umuhimu na faida za kunawa mikono mara kwa mara ili kutunza afya zao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.