Wednesday 11th, December 2024
@Jiji la Dodoma
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inatarajiwa kufanyika katika Jiji la Dodoma tarehe 8, Machi Mwaka huu.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanaadhimishwa kuanzia tarehe 02/03/2019 na kufikia kilele tarehe 08/03/2019. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "BADILI FIKRA KUFIKIA USAWA WA KIJINSIA KWA MAENDELEO ENDELEVU"
Shughuli zitakazofanyika katika kuadhimisha ni pamoja na kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General), kufanya maonesho ya shughuli za vikundi vya wanawake na kliniki ya kupima Afya vitakavyofanyika katika Uwanja wa Mashujaa.
Siku ya kilele tarehe 08/03/2019 maadhimisho yataanza saa 1 asubuhi kwa maandamano yatakayoanzia Uwanja wa Jamhuri kuelekea Uwanja wa Mashujaa ambapo mgeni rasmi atakuwa Mhe. Jenista Mhagama (WM-Sera, Bunge, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu).
Bofya hapa chini kuona ratiba kamili ya shughuli za maadhimisho.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.