Sunday 22nd, December 2024
@Shule ya Msingi Ng'ungugu - Kata ya Kikombo
Zoezi la upandaji miti 500 katika Shule ya Msingi Ng'unguju iliopo Kata ya Kikombo. Zoezi hili litajumuisha wananchi wa Kata ya Kikombo, Watumishi kutoka Ofisi Kuu ya Jiji na Viongozi mbalimbali wa Serikali. Zoezi hili linafanyika kutekeleza agizo la Makamu wa Rais Samia Suluhu alilolitoa wakati wa kampeni ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katamba na litahudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Godwin Kunambi, Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Jiji, watumishi kutoka Ofisi kuu ya Jiji na wananchi wa Kikombo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.