Wednesday 22nd, January 2025
@Viwanja vya Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imetangaza kuzinduliwa rasmi kwa Mradi wa Vituo vya Huduma Pamoja na mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa (Mb), Septemba, 6 2021 katika viwanja vya Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mkakati uliopo sasa ni kulifanya Shirika hilo kuwa kitovu cha Biashara Mtandao hivyo kufanya ushirikishwaji wa pamoja katika kutoa huduma kuwa ni jambo la muhimu.
Shirika la Posta litazindua rasmi huduma ambayo itazikutanisha taasisi mbalimbali za Serikali na kutoa huduma kwa pamoja ikiwemo NIDA, NSSF, RITA, TRA, PSSSF, NHIF, Halmashauri ya Jiji la Dodoma na nyinginezo ambazo zitatoa huduma kupitia ofisi za Posta nchini.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.