Saturday 14th, December 2024
@Nala
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo (Mb) anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Uzinduzi wa Shule mpya ya Msingi ya Chiwondo katika Kata ya Nala. Shule hii imejengwa na Mheshimiwa Anthony Mavunde, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu.
Pamoja na hao shughuli hii inatarajiwa kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mstahiki Meya wa Jiji, Mkurugenzi wa Jiji, Madiwani, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Jiji la Dodoma, wananchi, waandishi wa habari na wadau wa elimu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.