Monday 30th, December 2024
@Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge kesho anatarajia kuanza ziara katika Wilaya ya Dodoma Mjini. Ziara hii ni muendelezo wa ziara yake aliyoianza tarehe 10 - 19 Juni, 2019 ambapo alitembelea Wilaya za Chemba na Kondoa. Katika kumalizia ziara hii, Dkt. Mahenge atatembelea Wilaya ya Dodoma kuanzia tarehe 20 hadi 21 Juni, 2019.
Ratiba inayonesha, akiwa Dodoma mjini Mkuu wa Mkoa atakagua mradi wa shule ya mfano ya Serikali na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara eneo la Ipagala.
Kisha ataenda kukagua ujenzi wa madarasa 8 shule ya msingi Ihumwa na baadae msafara wake utaelekea Nzasa kukagua ujenzi wa shule ya msingi Nzasa. Msafara wa Dkt. Mahenge utaondoka Nzasa na kuelekea Nzuguni ambako atakagua miradi mikubwa ya Soko Kuu na Stendi ya Mabasi kabla ya kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara.
Katika siku hii ya kwanza ya ziara yake, Mkuu wa Mkoa atamalizia ziara yake kwa kwenda Kikombo ambapo atapata fursa ya kuongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara.
Siku ya pili, ratiba inaonesha kuwa Dkt. Mahenge atakutana na kuzungumza na watumishi wa Jiji la Dodoma katika ukumbi mkuu wa Jiji. Baada ya mkutano huo, mkuu wa mkoa ataondoka kuelekea Mpunguzi na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.
Baada ya mkutano huo, msafara wa Mkuu wa Mkoa utaelekea Mbabala ambako pia atakutana na kuzungumza na wananchi wa Mbabala kwenye mkutano wa hadhara.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa atamalizia ziara yake kwa kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Mlimwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.