Kupata masharti ya uendelezaji kwa matumizi yaliyokusudiwa
Kuandaa michoro ya awali kwa kuzingatia masharti yaliyotolewa
Kuwasilisha michoro inayokidhi viwango
Michoro yote ya majengo maalum mfano ghorofa, kumbi, taasisi, hospitali, biashara na viwanda iwasilishwe kwa kuanza na taarifa ya mazingira (Environmental Impact Assessment) na michoro ya awali (Preliminary drawings)
Baada ya kupata kibali cha ujenzi mhusika analazimika kukaguliwa hatua zote za ujenzi na kuhakikisha fomu ya ukaguzi inajazwa na kusainiwa na wataalam wa Halmashauri ya Jiji
Kila mmiliki wa kiwanja anatakiwa kupanda miti isiyopungua 10 (mitano ya kivuli na mitano ya matunda)