Serikali imeweka Mfumo wa Utoaji Vibali vya kusafiria nje ya Nchi kwa njia ya Mtandao ili kurahisisha na kuongeza ufanisi katika kushughulikia maombi ya Vibali.
Kipengele cha dharura kimewekwa kwa ajili ya safari za dharura tu ili kukidhi maombi ya wagonjwa pamoja na mialiko/safari za kiserikali za dharura. Hivyo, waombaji wanapaswa kutuma maombi yao siku 14 kabla ya safari zao za kawaida ikiwa ni muda wa chini kabisa.
Ili kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi, mtumishi wa Jiji la Dodoma anatakiwa kuwasiliana na Afisa TEHAMA wa Jiji ili asajiriwe kwanza kwenye Mfumo (eSafari) ndipo apate nafasi ya kuingia kwenye mfumo na kujaza fomu ya maombi. Inaweza kuwa ni maombi ya kawaida ama ya dharura kutegemeana na uhitaji.
Kwa msaada zaidi wasiliana na Afisa TEHAMA ye yote wa Jiji la Dodoma.
MAELEZO YA AWALI KWA MWOMBAJI WA KIBALI CHA KUSAFIRI
MUHIMU:
Kusoma Mwongozo wa Mtumiaji wa Bofya hapa: MWONGOZO WA MFUMO WA VIBALI VYA KUSAFIRI (eSafari)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.